Injili ya Yohana sura ya 1
Injili ya Yohana (Biblia Swahili Union Version)
Nyimbo inayoanza katika Injili ya Yohana 1:1-18
Mwanzo wa Injili ya Yohana ni yakushangaza sana. Kwa sababu mwandishi ananza bila ya kuwa na onyo lolote mwandishi anaongoza wasomaji wake au badala ya wasikilizaji kuwa katika urefu wa ajabu kabisa. Aya kumi na nane za kwanza zinaunda kinachojulikana kama “nyimbo za logos (neno)”. Zaburi yenye kupendeza kuhusu neno la Mungu na jinsi neno lilivyofanyika kuwa mwili.
Sehemu ya kwanza katika nyimbo inayoonyesha Agano la Kale ni ya kawaida kwa wasomaji wote wa Biblia. Kwa kushangaza, Injili ya Yohana huanza karibu kwa njia sawa na hadithi ya uumbaji. Ujumbe upo wazi kabisa: tunazungumzia kuhusu suala la msingi sana hapa.
Pia kuna eneo katika Agano la Kale, ambalo linafanana na mwanzo wa Injili ya Yohana. Ili kuweza Kutambua inahitaji uwe na ujuzi mzuri wa Agano la Kale. Tukisoma katika Mithali 8. Inatoa picha yenye kupendeza ya hekima ambayo ilikuwa chombo cha Mungu katika uumbaji. Tunazungumzia juu ya hekima fulani, ambalo ni neno la maandiko. Nyimbo ya neno inatufundisha kuona kwamba hekima ni Yesu ambaye ndiye Mwana pekee wa Mungu. Kutokana na sehemu hii maalumu katika Biblia, Kanisa linakiri kwamba “Kwa njia yake vitu vyote vilifanywa; bila yeye hakuana chochote kilichofanywa ambacho kimefanyika. “Kwa hiyo, kina kirefu cha nyimbo ya Neno” huanza kufungua. Mwana wa pekee wa Mungu alikuja kutoka utukufu wake ili kuleta nuru ndani ya giza la ulimwengu.
Watu wengi ambao waliishi na Yesu hawakuweza kuona utukufu wake. Lakini Kwa wale ambao Mungu aliwapa uwezo wa kuona, walitambua kwamba Mungu mwenye rehema alikuwa ameshuka ili kuishi kati ya watu wake. Nini maana yake inaelezwa katika aya ya mwisho ya wimbo kwa njia ya kushangaza: hapo awali (katika mstari wa 14), mwandishi huzungumzia“ Mwana pekee kutoka kwa baba”. “Yesu ni Mungu pekee”.
Haki kutoka mistari ya kwanza tunakutana na theolojia ya kawaida ya Yohana. Moja ya jozi muhimu ya neno ni “mwanga” na “giza”. Hasa jozi moja neno linapatikana mara kwa mara kwenye barua ya kwanza ya Yohana. Kwa sababu ya dhambi, ulimwengu wote uliishi katika giza lenye kusikitisha. Lakini wakati Kristo alipokuja duniani, ulimwengu ulikutana na nuru kubwa sana inayoonekana na wengine, lakini si kwa kila mtu. Aliyempata Kristo, amekwisha kupita katika Giza na kuwa katika mwanga, au kama vile Yohana anasema mahali pengine –kutoka kifo kwenda kwenye uzima.
Shahidi wa Yohana Mbatizaji 1:19-28
Katika injili zote nne, Yohana mbatizaji ni mhusika mkuu mhimu sana. Mwinjilisti wa Kwanza Marko ananza kueleza shughuri za Yesu kwa kueleza jinsi Yesu alikuja kwa Yohana Mbatizaji na kubatizwa. Mwinjilisti Yohana kwa sehemu ya ushahidi wake ndani ya “nyimbo za neno” inaonekana kwamba kwa wakati huu Mwinjilisti anafkria wasomaji wake kuwa tayari wanajua mengi. Husema hata juu ya ubatizo wa Yesu, lakini anaelekeza kipaumbele chake kwa ushahidi wa Yohana mbatizaji. Huu ni mfano mmoja tu wa kugusa nguvu ya sanaa ya mwinjilisti wa nne: si lazima kufunua kila kitu; isipokuwa msingi wa matukio na maana yake ni mhimu sana kuwaambia.
Wale waliokuja kwa Yohana Mbatizaji walikuwa “Wayahudi”. Hilo ni neno ambalo Yohana alitumia hasa wakati wa kuwaeleza Waisrael ambao walimkataa Kristo, maranyingi bila kutaja makundi yoyote au vyama Fulani. Ilikuwa wakati baada ya uharibifu wa Yerusalemu, na tofauti kwa mfano kati ya wafuasi wa mafarisayo, masadukayo na wafuasi wa Herode, walikuwa wamepoteza umhimu. Yohana Mbatizaji alijaribiwa, na majibu yake yalikuwa wazi kuonyesha njia yetu, waamini wa baadaye. Yeye si Kristo au Eliya, wala Nabii Musa ambaye alikuwa ametabiriwa kuja (Kumbukumbu la Torati 18:18). Mbatizaji alikuwa “Sauti ya kilio” ambayo Isaya alikuwa ametabiri. Kazi yake ilikuwa ni kuwaambia juu ya kuja kwa mtu mkubwa zaidi.
Kuna mambo ya kuvutia katika ushuhuda wa Yohana Mbatizaji. Baadhi ya Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji waliendeleza shughuli zao na mikusanyiko baada ya mwalimu wao kufa. Kwa kweli mwinjilisti aliwaeleza pia maneno yake kwao. Kipengele kingine cha kuvutia ni mfululuzo wa maswali- hasa maswali mawili ya mwisho. Yohana alikanusha kuwa yeye ni Eliya (Mathayo 11:14), au kulingana na Mathayo yeye alikuwa ni Eliya (Mathayo 11:14), au angalau alifanya kwa roho ya Eliya. Wa tatu alisubiri tabia zilizokuwa za nabii aliyeahidiwa na Musa. Matarajio ya kumwona kwake yalikuwa makubwa, sio tu kati ya Wayahudi, bali pia kati ya Wasamaria. Yohana alikata sifa hizi zote, na badala yake alitaka kuwa shahidi wa Yule aliyekuja.
Mwanakondoo wa Mungu 1:29-34
Siku iliyofuata, Yohana alifafanua ushuhuda wake. Sasa alikutana na Yesu na Mungu akamfunulia kiini cha kweli cha mtu huyo. Yesu ndiye sababu Yohana alianza kufanya kazi yake. Mtangazaji wa kibatizaji anasema neno la Mungu lililokuwa Mwili.
Wakati akizungumza juu ya “Mwanakondoo wa Mungu”Yohana alikuwa na maneno mawili ya Agano la Kale katika akili. La kwanza linahusiana na Pasaka. Wakati Mungu aliwaachilia watu wake kutoka utumwa wa Misri, alitoa amri ya kuwa na chakula cha jioni cha Pasaka. Kiini cha chakula kilikuwa ni kondoo. Mungu aliwaambia watu wake kuua mwanakondoo na kunyunyizia damu yake juu ya miimo ya milango kuingia kwenye nyumba zao. Wakati mharibifuu wa Mungu aliyetumwa na Mungu aliua wazaliwa wa kwanza wa Misri, damu ya mwanakondoo ilikuwa ni kama alama inayoonyesha ambapo watu wa MUngu waliishi. Wazaliwa wao wa kwanza waliepuka hatima ya kuawa (Kutoka 12). Sehemu hii pia ni nyuma ya matukio ya baadaye (Yohana 19: 36). Sehemu nyingine inayozungumzia juu ya mwanakondoo katika Agano la Kale ni kitabu cha Isaya, sura ya 53. Kwa hiyo, tayari nusu ya kwanza ya sura ya ufunguzi ya injili inamweka Kristo mahali pake. Yesu ni mwanakondoo na mwana wa MUNGU mwenyewe, na wakati huo huo yeye anaokoa watu wenye dhambi kupitia damu yake mwenyewe.
Kutokana na na Injili ya nne, wanafunzi wa kwanza wa Yesu walikuwa awali wanafunzi wa Yohana Mbatizaji. Hiyo ni kwa njia iliyothibitishwa pia na Luka, ambaye anasema kuwa badala ya Yuda, mtume mpya alipaswa kuchaguliwa kati wale waliokuwa wamefuatana na Yesu “tangu Yohana alimbatiza” (Matendo ya Mitume 1:22).
Yohana anaelezea matukio kwa kina, na kwa namna ambayo ni vigumu kuchanganya na Injili pacha. maana kuu ni karibia inafanana sawa: Yesu anawaalika wanafunzi 12 (Yohana 6:67) na Petro ana nafasi maalum kati yao. Wanafunzi wawili wa kwanza walisikiliza ushauri wa Yohana na kumfuata Yesu. Mmoja wao alikuwa Andrea na mwingine jina lake halikutajwa. Kanisa la kawaida linafikiri kwamba alikuwa mwandishi wa Injili hii. Tarifa haijulikani sana, lakini sio uongo. Na Andrea, pia Simoni alijiunga na Yesu, ambapo Yesu alimpa jina la Kefa, katika lugha ya kigiriki Petros na kifini Kallio. Wanainjili pacha waliunganisha jina la kukiri kwa Petro (Mathayo 16:16).
Yesu alitoka bonde la MtoYorodani akaenda Galilaya. Katika Safari, Filipo naye akamfuata na kumwambia Nathaniel kwamba amemwona Kristo. Nathaniel alikuwa na wasiwasi, lakini hivi karibuni alitambua kuwa Yesu aliona kushangazwa kupitia maisha yake yote. Kwa mara ya kwanza kulikuwa na mvutano kati ya imani ya miujiza na imani ya kweli. Nathaniel alianza kumfuata Yesu kwa sababu ya miujiza. Hiyo ilikuwa bila shaka, kukubalika kabisa, lakini imani inayotokana na miujiza inabakia kwa hakika. Kukiri ya kweli na a kweli ya kiimani inaweza kusikiwa Kama kutoka kwa Martha. Inaonekana kwamba Martha alisema kabla Yesu hajamfufua kaka yake Lazaro kutoka kwa wafu: “Naamu, Bwana, nimeamini kwamba Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, hata Yeye anayekuja ulimwenguni.” (Yohana11:27). Wanafunzi wa Yesu hawakuwa na imani sawa na hiyo ambayo inashirikiana na ushuhuda wa Martha au katika nusu ya kwanza ya sura ya kwanza katika Injili ya Yohana, pamoja katika mwanzo wa nyimbo na katika ushahidi wa Yohana Mbatizaji. Lakini wanafunzi waliruhusiwa kukaa kundi pamoja na Yesu na kujifunza zaidi na zaidi.