Injili ya Yohana sura ya 5 – Baba na Mwana ni mmoja

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Emmanuel Samwel Sitta

Yesu pia huponya siku ya sabato Yoh 5:1-18

Kulikuwa na wagonjwa wengi na walemevu karibu na birika la betisaida. Katika wakati wa Yesu, watu hawa walikuwa wanakabiriwa na taabu nyingi katika familia zao ambazo hazikuweza kuwahudumia.

Muujiza wa uponyaji husemwa kwa ufupi na kwa uwazi. Ijapokuwa Yohana hakusisitiza wakati huu, uponyaji wa ajabu wa watu wenye upofu unaounganishwa na Isaya 35:6 “ndipo mtu aliyekilema atarukaruka kama kurungu”. Mungu alikuwa ameahidi kwamba wakati wa wokovu ungekuja mara moja. Na vipofu wataona, viziwi wataisikia na walemavu watarukaruka kuzunguka katika jubilee. Wakati mtu ambaye ameteseka kutokana na ugonjwa kwa miaka 38 anatembea na kuzunguka akiwa amebeba kitanda chake, ilimanisha ya kwamba, ahadi kubwa za Mungu zilikuwa zinatimia.

Hata hivyo kwa kufanya hivyo Yesu alikuwa ametukana jambo takatifu sana ambalo mafarisayo walilijua. Siku ya uponyaji ilikuwa ni sabato. Na kwa mujibu wa sheria ilikuwa imepigwa marufuku kubeba mali yeyote siku hiyo. Yesu hakumwambia mtu huyo aende nyumbani, lakini tu alimwambia abebe godoro lake. Inaonekana kama Yesu alitenda kinyume na mafundisho yaliyoenea kwa makusudi. Na hii ikawa imesababisha hasira kubwa.

Sababu ambayo Yesu aliitoa kwa ajili ya hatua yake ilifanya hasira ikaongezeka. Mungu hufanya kazi daima, siku kwa siku. Mwana wa Mungu hufanya sawa kabisa katika ulimwengu. Mpangilio wa sabato uliomfunga Yesu kama vile humfunga Mungu. Baada ya mafundisho haya, Ni mara ya kwanza katika Injili ya Yohana kwamba tunaona mapema matakwa na mikakati ya Wayahudi kuhusu kumuua Yesu.

Baba na Mwana ni mmoja Yoh 5:19-23

Sura hiyo inaendelea na mwongozo mrefu wa Yesu. Maneno ya kwanza ya hotuba ni maelezo ya maneno ambayo, yaliwafanya Wayahudi wawe na hasira; yaani, Yesu kuwa sawa na Mungu. Hatua ya msingi ya Yesu ni kwamba Yeye ni mwana wa Mungu, na kwamba baba amempa mamlaka yote. Mwana huona matendo ya Baba yake na yeye mwenyewe anafanya hivyo. Yeye si chini ya hukumu ya watu, lakini kinyume chake Baba ametoa uwezo wake kwa Mwana. Mapenzi ya Mungu ni kwamba Mwana anaheshimiwa kama Baba. Anayemheshimu Mwana, anamuheshimu na Baba pia. Injili ya Yohana sasa inasema wazi ujumbe wa Kikristo. Kwa njia hiyo inaelezea yale yaliyotajwa katika utume mkuu kwa muda mfupi na kwa wazi:

“Nimepewa mamlaka yote Mbinguni na duniani …”
(Mathayo 28:18)

Msingi wa mamlaka ya Mwana ni haki ya hukumu 5:24-29

Mungu ametoa mamlaka kwa mwanae, na kunakusudi la wazi kwa hilo. Yesu tayari amekwisha kurahisisha maelezo ya kusudi hili katika Yohana 3:16. Mungu alitaka kuhamisha watu chini ya hukumu na kifo kwa uhuru na maisha.

Ni kawaida kwa Injili ya Yohana kwamba hukumu inatokea kwa njia mbili. Inatokea mwishoni mwa nyakati, lakini pia imeshakwisha kutokea tayari, tunaposikia maneno ya Yesu. Yohana anazungumza kidogo juu ya hukumu ya mwisho, lakini bado inaonekana kuwa imeshakuwa dhahiri. Kutakuwa na nyakati ambapo kila mfu katika kaburi atasikia sauti ya Jaji Mkuu na kukutana na hukumu. Wale ambao wamefanya mema, watahukumiwa kwa furaha ya milele. Wale ambao wamefanya kinyume na mapenzi ya Mungu, watahukumiwa kwa hukumu ya milele.

Historia ya hili ni maono makuu ya Danieli (Danieli 7: 13, 12: 1-3), ambapo hakimu “ni kama mwana wa mwanadamu” , hivyo ni kama mtu. Kwa sababu ya maneno haya watu walitarajia “Mwana wa mtu” kuja na kuhukumu. Yesu anatangaza kwamba yeye, mwana wa Mungu, ni aliyetabiriwa “mwana wa Mtu” na ni hakimu wa mwanadamu.

Kipengele kingine, kwa kawaida kuhusu injili ya Yohana hasa, ni kwamba hukumu haitoi tu mwisho wa nyakati. Baba amempa Mwanawe mamlaka. Ndiyo sababu hatuna kusubiri hukumu au ukombozi hadi hukumu ya mwisho. Wakati ambapo wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu na kuishi, tayari imeshakwisha kuwepo hapa. Hatima yetu ya milele imeshaamuliwa tayari hapa na ni sasa, kulingana na uhusiano wetu na Kristo. Ikiwa sisi tuna Kristo, hakuna mauti bali sisi tuna maisha. Ikiwa hatuko pamoja na Kristo, hakuna uzima lakini kuna kifo.

Ni nini kinathibitisha kwamba Yesu anasema kweli? 5:30-45

Maneno ya Yesu ni dhahiri naya kushangaza kwa Wayahudi kuyasikia. Wanawezaje kujua kwamba alikuwa akisema ukweli? Kulikuwa na mashahidi wengi walioshuhudia jambo hili:

  • Yohana mbatizaji alitoa ushahidi juu ya Yesu, kama inavyoelezwa katika sura ya kwanza na ya tatu.
  • Miujiza ya Yesu inaonyesha kwamba alitumwa na Mungu. Tunahitaji kulinganisha na Isaya 35, kwa mfano, kama historia.
  • Mungu mwenyewe anashuhudia juu yake katika neno- katika Agano la Kale, kama tunavyosema.

Mashahidi hawa watatu watakuwa sababu kubwa sana ya kukubali idhini ya Yesu na kumwamini. Hata hivyo, Wayahudi hawakufanya hivyo, na ndivyo sababu hawakuweza kupata uzima.

Mashahidi wote watatu wana mambo mazuri sana yanayohusiana nao. Yohana ana nafasi maalumu ambayo inaweza kuonekana katika Injili zote.

Maajabu ambayo Yesu alifanya yalikuwa mengi zaidi kuliko kuponya mtu mmoja.
Wanasimama mashahidi ambao walionyesha kuwa Yesu ni nani na anasema nini.

Shahidi wa tatu ni mhimu zaidi. Mungu anashuhudia Yesu-hasa katika Agano la Kale. Hii ni jinsi Yesu na Mitume walivyosoma Agano la Kale. Wayahudi hawakuweza kumpata kwa mfano katika vitabu vya Musa (Kutoka Mwanzo hadi kumbukumbu la Torati), lakini Kanisa la kwanza ilimtumia Yesu Kristo kama ufunguo wa Biblia nzima.

Katika mistari 37-40, ushahidi wa Baba na neno la Biblia (Agano la Kale) ni sawa. Kanisa letu linakubali kwamba Roho Mtakatifu amesema kwa kupitia mitume na manabii na hii ndiyo jinsi Biblia nzima inavyoonekana kuwa neno la Mungu. Yeyote anayekataa hili amekwenda mbali na kujitenga na ukweli.