Ukristo unatofautianaje na dini zingine?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Dini zingine hujibu swali jinsi ya kuishi maisha mema na kumkaribia Mungu. Ukristo hutoa jibu tofauti. Mtazamo si kwetu ila yale Mungu amefanya.

Dini zingine hukuongoza utakavyo mtii Mungu, kutenda mema au kujaribu uwezavyo ili uweze kubarikiwa na uweze kufikia wokovu. Ukristo una ujumbe tofauti: Kila kitu kilifanyika tayari kwa Baraka na wokovu. Hatuwezi kujikokoa ila Yesu alituondelea dhambi. Tumeokolewa kwa neema, kwa kupokea zawadi tuliyopewa na Mungu. Hatuhitaji kufanya chochote ili kufanya Mungu atupende. Anatupenda kabisa. Tunaweza kutulia katika imani katika Mungu na kuwatumikia wengine na upendo ambao Mungu anatupa.

Msingi wa Ukristo ni neema ya Mungu. Ni neema tu katika Kristo ambayo itatuokoa. Dini zote ambazo zimejengwa juu ya uwezo wako na matendo huelekea upotevuni na kukata tama.

Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
(Yohana 14:6, SUV)

Bwana, ninataka kukuamini lakini mimi ni mnyonge na nina mashaka. Nizaidie!