Imani inafananaje katika maisha ya kila siku? Na ninawezaje kumfuata Yesu?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Muumini ni msharika katika Kanisa. Wakristo wanaunganishwa na wakristo wengine; kusikiliza neno la Mungu, kuomba, na kushiriki meza ya Bwana tena uunganishwa kwa kusudi maalumu. Yote haya yanaimarisha, na kulinda imani. Roho Mtakatifu yupo kutuimarisha sisi.

Amri za Mungu zinatuhusu sisi sote. Kama mkristo hatuwezi kuzidharau Amri za Mungu na mapenzi ya Mungu baba yetu wa mbinguni.

Kila mmoja wetu hapa ana wito wake, na Mungu anataka tuwe waaminifu katika kuhudumia watu wanao tuzunguka. Hata hivyo wakati tunapokumbana na mahitaji ya maisha haya, mara moja tunatambua kuwa mwisho wetu kama binadamu na kwamba nguvu zetu hazitoshi. Tujisikia wadhaifu. Na hivyo tunajaribu kufanya kile kilicho kinyume na Amri za Mungu na dhambi.

Asili ya ubinadamu wetu, mwili wakati wote unatuingiza katika dhambi na kufanya yale yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu haijalishi wewe ni mkristo au la! Hivyo tunahitaji msamaha wa Mungu usio na kikomo, kuomba na nguvu zitokazo kwa neno la Mungu.

Maisha katika imani hata hivyo si kukana vitu na kujitahidi kuwa bora. Kama Mkristo tunaishi kama watoto wa Mungu ndani ya uhuru na usalama ndani ya Neema yake. Katika Kristo Yesu tunapewa imani, tumaini na upendo kama zawadi. Hii ndiyo sababu Mkristo anapenda kusogea karibu na Yesu.

"Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu."
(Yoh 15:9, SUV)

Ombi: Bwana Mungu nisogeze karibu na Yesu katika njia zako. Usiniaje nipoteze njia yangu.