Kifo, Mbinguni

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mwanadamu aliumbwa kwa kuishi milele. Kuvunja mapenzi ya Mungu kifo kikaja, na hakika kinatuhumiza sisi sote. Hata hivyo kifo hikitashinda mwisho.

Katika kifo, muda wetu wa rehema unafika mwisho. Katika ulimwengu huu ulioumbwa tunaweza kuishi kwa zawadi ya Mungu. Hata kama hatumjali Mungu kabisa. Kinachotokea, hata hivyo, wakati tunapoteza pesa zetu, uzuri, nafasi zetu katika kazi, afya na maisha? Nini kinatokea tunapokutana na Mungu aliye uchi katika dhambi zetu? Yeye aliyetupa uzima atatuuliza tumeutumiaje? Hatutakuwa uchi katika kipindi hicho. Biblia inatufundisha kwamba katika imani tutavikwa mavazi meupe, nayo ni haki ya Kristo. Tuliopewa katika ubatizo. Katika ni imani, inamilikiwa.

Nini kuhusu baada ya kufa? Waliokufa wamelala Kiroho kabla ya ufufuo wa siku ya mwisho? Biblia inatufundisha kwamba katika kifo mtu anakwenda katika ukweli mwingine. Sio lazima kujua urefu wa kipindi hicho, lakini kipindi hiki cha kusubiri ni cha furaha au cha huzuni au wakati wa dhiki. Dhamiri ikiwa nzuri kila mmoja anajua nani anasubiri, ni vizuri kusubiri.

“Lakini ndugu , hatutaki msifue habari zao waliolala mauti , msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini maana ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye."
(1 Thesalonika 4:13-14, SUV)

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kutoka kwa Yesu. Ni asili kwamba tunaogopa kifo. Kifo na washirika wake- magonjwa, ajali majanga yote ni ya muovu, si sehemu ya uumbaji wa Mungu. Kifo kwa hakika si cha asili na hutakiwi kuwa rafiki nacho. Paulo alisema “kifo ni adui wa mwisho. lakini kazi ya Yesu ni ushaidi imara kwamba kifo na washirika wake hawatashinda.”

Yesu ameshinda kifo, na wewe kama mtoto wake utatokea kupitia kifo kama mshindi. Sikia kwa makini wewe mwenyewe. Hakikisha unajikabidhi kwa Yesu. Atakikabili kifo chako moja kwa moja. Hata kama unaogopa bado. Fanya kama vile mtoto mdogo wanavyofanya anpokuwa na hofu: Mkikimbilie baba yako. Anatuliza hali. hata kama usiku ni mrefu na wa giza. Hisia hushindwa mara nyingi, lakini Imani ambayo inaamini katika Neno la Mungu, haitashindwa.

“Yesu akamwambia, mimi ndimi huo ufufuo, na uzima aniaminiye mimi,ajapokufa atakuwa anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa milele, je! Unayesaidika hayo?"
(John 11:25-26, SUV)

Ombi: Mungu bado kifo kinaniogofya. Utakuwa pamoja nami?
Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kifo si mwisho wa yote.
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa ,cheupe na yeye aketiye juu yake , ambaye Nchi na Mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana, Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi. Na vitabu vikafunguliwa , na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha Uzima, na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawasawa na matendo yao" (Rev. 20:11-12, SUV)

Itakuwa furaha kuu kuwaona huko Mbinguni. Nadhani ni ushauri mzuri kuamini wengine na kuwa na shaka kujihusu mwenyewe. Waache jamaa zako waliokufa katika wangalizi wa Mungu na uombe kwa ajili yao mara moja au mbili. Wewe mwenyewe uamini katika mshindi wa kifo. Unaweza kujifariji mwenyewe kwamba kwa Mungu hakuna yeyote amekufa. Kwake kila mtu ni hai (mzima) kwa sababu yeye hafungwi katika sheria za ulimwengu huu.

“Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai, nilikuwa nimekufa tazama ni hai hata milele na ni nazo hizofunguo za kifo na kuzima”
(Ufunuo 1:17-18,SUV)

Mungu ninaweka wapendwa wangu waliokufa katika mikono yako salama.
Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ndio ipo. Agano la kale linasema kwa kina kuhusu mahali baada ya kufa, lakini kati ya kipindi cha Agano jipya inatoa mwanga hata katika ukweli wa giza hili. Yesu alisema jehanamu haikuumbwa kwa ajili ya mwanadamu ila ni kwa ajili ya shetani na malaika zake. Unaelezewa kama Jehanamu ya moto wa milele, ziwa la moto Giza, utengano, kilio na kusaga meno. Wakati hatuwezi kuelezea ni vipi tunafikiri kuhusu mtazamo wa kuzimu, tunaweza kutazama katika tafsiri hii: Kuzimu na utengano wa milele na Mungu na uzuri wote wa Mungu. Mkristo hatakiwi kuwa na mvuto wa kuzimu, zaidi sana uepuke kuwa huko. Tunatakiwa kukumbuka kuwa Yesu hakuja katika ulimwengu huu kutuogopesha kuhusu kuzimu bali kutukomboa kutoka ajili ya kwenda Mbinguni. Wewe pia!

“Kisha atawaambia na wale waliopo mkono wake wa kushoto, ondokeni kwangu, mliolaaniwa mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilishi na malaika zake.”
(Mathayo 25:41, SUV)

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia haijatupa kijiografia mahali mbinguni ilipo. Mbinguni ni pale ambapo Mungu anapokaa katika ukamilifu wake. Biblia inasema;
“Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti amekaa katika Nuru isiyoweza kukaribiwa, wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona, Heshima na uwezo una yeye hata milele Amina” (1 Timotheo 6:16, SUV)
 Hivyo basi hatuwezi kumfikia Mungu au Mbingu kupitia nafsi yeyote katika mpango wa kuchunguza wala kupitia akili zetu.

Yeye mwenyewe ametoka katika sehemu aliyojificha na kujifunua kwetu, kila tunachohitaji kujua kuhusu mbinguni. Biblia kwa mfano katika kitabu cha Ufunuo kuna maelezo mbali mbali kuhusu picha za mbinguni. Hizi picha haziwezi kulinganishwa kutoka katika picha moja nzuri. Ni kwa jinsi gani chumba kama mji umejaa barabara za dhahabu unavyoonekana? Au ni vipi kuabudiwa pasipo mwisho kunavyoonekana? Vipi kuhusu bustani, ambazo uzuri wake ni mzuri haijawahi kuonekan. Hii ni nini kwamba Mungu mwenyewe atayafuta machozi yetu. Mwalimu moja wa zamani wa kanisa alisema hivi kuhusu mbinguni” furaha ya Mungu inaonekana; kwangu mimi hiyo ni tayari sababu tosha kutaka kuona yote hayo!”

“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.”
(Ufunuo 21:3, SUV)

Ombi: Mungu anataka kwenda mbinguni nichukue mimi huko