Yesu

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Haya ndiyo Wakristo wa kwanza walikiri. Waliamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu aliyekuja duniani kama mwanadamu. Kuna kifungu kinachosema “Yesu ni Bwana” kinadhaihirisha hakika imani yao.

Injili ndani ya agano jipya zinatuambia habari njema kuhusu Yesu, jinsi alivyochukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu na kuzaliwa na bikira Maria, na jinsi alivyoishi, kufundisha na kutenda miujiza mingi. Yesu ni nani, mateso yake, kifo chake na kufufuka kwake siku ya tatu viko katika msingi wa Ukristo.

Je! Yesu ni nani kwako?
Ufahamu wako juu ya Yesu, na yeye ni nani kwako inaamua hali yako umilele. Kwa hiyo ingiza mikono yako katika bibilia na tafuta kujua zaidi.

Kwa kufa kwake msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka kwake kutoka kwa wafu, Yesu alifanya njia kwetu ya kumfhamu katika wenyewe. Ni kupitia Yesu tu tunaweza kuokolewa na kuwa na uhusiano na Mungu.

“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.”
(Matendo ya mitume 4:12 SUV)

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Wasomi na wanahistoria hawawezi kukataa historia ya Yesu.
Mtu aitwaye Yesu alikulia Galilaya katika mji utwao Nazareti. Hivyo mara kwa mara alijulikana kama Yesu wa Nazareti. Yesu alifundisha katika sehemu nyingi, alikusanya wafuasi, ambao walikusanya mafundisho yake na kuyasambaza. Takribani mwaka wa 30 huko Yerusalemu Pontio Pilato alitoa amri Yesu auwawe. Wanahistoria wanakubaliana na kweli hizi.

Lakini Yesu alikuwa ni nani? Nawezaje kumfahamu vema? Majibu ya maswali haya yanaweza kupatikana ndani ya Biblia, zaidi ndani ya agano jipya.

“Mwanzo wa injili ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu.”
(Marko 1:1 SUV)

Ombi: Yesu! Wewe Ni Nani?
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Yesu alipawa adhabu ya kifo kwa sababu wazee wa Kiyahudi walidai alimdhihaki Mungu. Kwa mafundisho na miujiza yake, Yesu adhibithisha kuwa yeye ni mwana wa Mungu aliyeshuka kutoka mbinguni. Kulingana na na sheria ya Musa mtu anayedai kuwa yeye ni Mungu alihesabika kama anakufuru, na nilazima apate adhabu ya kifo.

Hata hivyo ni Warumi waliooweza kutoa hukumu ya kifo. Mtawala Pontio Pilato hakuwa haja malumbano ya kidni kati ya viongozi wa kiyahudi. Hivyo Pilato hakushawishiwa, hata hivyo alitoa hukumu ya kifo kwa kulazimishwa ili Yesu asulubishwe.

Yeyote anayesoma habari ya kifo cha Yesu na kusulubishwa kwake katika injili anaweza kushangaa kwa nini mtu mwema hivi na asiye na makosa afe kifo cha kusikitisha hivyo. Kwa nini Yesu hajitetea kwa uongo?

Tunapata majibu kutoka kitabu cha “Isaya 53" – cha ajabu haya yaliandikwa miaka mia tano kabla ya kifo cha Yesu. Kama wakristo tunaamini hili na mistari mingine katika Biblia inavyosema, kwamba haya yote yalikuwa ni mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Yesu alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, Mungu alimtuma mwane Yesu mwanaye wa pekee ili afe na kuteseka ili sis tusiteseke hivyo Alikuwa upatanisho wa dhambi zetu.

"bali alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kupigwa kwake sisi tumepona sisi sote kama kondoo tumepotea kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote”.
(Isaya 53:5-6 SUV)

Ombi: Bwana Yesu siwezi kuelewa mateso uliyopitia lakini nina amini kwamba dhambi zangu zimesamehewa.
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ni sehemu mbili zinatueleza tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?

Matukio mawili ya mazimulizi yamezungumziwa tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?
Injili ya Mathayo inatuambia jinsi walinzi katika kaburi la Yesu walipewa rushwa na kupewa maelezo ya kusema kwamba wanafunzi wake walikuja usiku na kuiba mwili wa Yesu. Uongo huu unaendelea hata leo na unaendelea kuboreshwa na kuwa kisasa. Maelezo ya leo ni kwamba kifo cha Yesu kilisababisha mkanganyiko wa kiakili kwa wanafunzi. Hivyo njia moja tu ya kuendelea kuishi ni kutengeneza imani, kuamini kwamba Yesu alifufuka katika wafu na kupitia imani anaishi katika roho.

Agano jipya hata hivyo linatuambia kwamba kuna watu wengi waliokutana na Yesu katika hali ya kimwili. Wanawake katika kaburi, wanafunzi waliokuwa wamefunga milango kwa hofu, watu wawili katika safari ya Emau n.k. Tomaso mwenye mashaka alipata nafasi ya kugusa majeraha ya Yesu. Watu hao wote walikuwa na vitu vinavyofanana: walikuwa na muda mgumu wa kuelewa na kukubali kwamba hakika Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.

Baada ya kufufuka kwake Yesu hakujionyesha kwa washtaki wake au ulimwengu mzima ni kaburi tupu tu ndilo lilidhihirisha hivyo. Mwili wake haukuwepo kaburini.

Hakuna kazi ya kuweza kuhakiki hiyo kazi au kutoa sababu ambayo inaweza kumshawishi mtu kuhusu ufufuko wa Yesu- imani huja unapokutana na Yesu. Yesu yuko mbinguni na baba yake, lakini neno lake-Biblia linazidi kuzungumza na watu ulimwenguni. Kanisa lake ni hakikisho kwamba Yesu yu hai.

”Yesu akamwambia kwa kuwa wewe umeniona, umesadiki; waheri wale waio ona wakasadiki.”
(Yohana 20:2a SUV)

Ombi: Yesu wasema kwamba unaishi. Unanisikia ninapoomba?
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Njia sahihi ya kupata kumjua Yesu ni kusoma kuhusu yeye ndani ya Agano jipya ambacho ni kitabu cha chapekee ambacho kilichoenea ulikwengu mzima yaani Bibilia. Tunaweza kusoma kile ambacho alifundisha, nini alifanya akiwa duniani na kusoma hadhithi ya watu waliomjua Yesu na kutembea naye. Biblia inatuambia maisha ya Yesu kifo chake na kufufuka kwake.

Kuna baadhi ya barua zimeandikwa na mitume katika Agano jipya vile wakristo wa kwanza na kanisa la kwanza lilivyokuwa. Watu hawakukutana na Yesu moja kwa moja lakini walimjua yeye walimsoma na kusikia habari zake.

Hata leo kuna watu wanomjua Yesu. Unaweza kuwapata kanisani, mahali watu wanapokusanyika pamoja kujifunza kuhusu Biblia kuomba na kushiriki katika meza ya Bwana, tafuta kanisa na nenda moja kati ya hilo - huwezi kukuta tu watu wanaomjua Yesu lakini unaweza kupata kumjua Yesu wewe mwenyewe.

“basi Yesu akawajibu akasema mafunzo yangu siyo yangu mimi ila ni yake aliyenipeleka mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake atajua habari ya yale mafunzo kwamba yatoka kwa Mungu au kwamba mimi na nena kwa nafsi yangu tu.”
(Yohana 7:16-17 SUV)

Ombi: - Yesu nataka kuwa na uhusiano na wewe. Jidhihirishe kwangu.
Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Kila mkristo anaushuhuda wake jinsi alipata kumjua Yesu. Mmoja aweza kupata mafunuo usiku, mwingine ilimchukuwa miaka mingi kupta kuamini na mwingine alimjua Yesu tangia utoto wake. Hakuna ushuhuda uliyomzuri kuliko wa mwingine. Hata hivyo nini kiliwafanya wawe wakristo kwa pamoja ni kwamba Bwana Yesu alifungua mioyo yao kupokea imani.

Hapa kuna ushauri mdogo kuhusu wale ambao wanaotaka kujua jinsi ya kuwa Wakristo: Acha kutoka kutoka kwa Mungu. Fungua masikio na sikiliza nini Bibilia inafundisha. Angalia yale Yesu amefanya kwa ajili yako. Mungu anakupenda. Yesu alikufa msalabani kwa ajili dhambi zako. Wewe ni mpendwa wa Mungu wako. Amini tu na mshukuru Mungu.

Unaweza kuomba: ”Yesu mwana wa Mungu nihurumie mimi mwenye dhambi”. Kulingana na Biblia Mungu atasikia maombi yeko na atakusamehe dhambi zako zote.Amehahidi kukusamehe katika Yesus Kristo.

Imani si kuhusu hisia ni kuhusu kuamini katika moyo kwamba Yesu ameniokoa. Muhimu ni kwamba unamwamini nani. Yesu atakuokoa. Wokovu ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kwa imani tunapokea zawadi hii.

Kama umebatizwa umekuwa muumini maana umerudi nyumbani tena na kuwa na uhusiano na Mwokozi wako. Tafuta Kanisa pale utasikia msamaha wa dhambi na kushiriki Meza ya Bwana na wakristo wengine.

Yesu anawaita kwake kila mmoja uwe umebatizwa au hujaptizwa, katika ubatizo tulisafishwa na kuunganishwa na Wakristo wengine.

(Nini kitatokea kama sikubatizwa?)

“Kwa kuwa kila atakaye liitia jina la Bwana ataokoka.”
(Warumi 10:13 SUV)

Ombi: - Bwana Yesu kristo mwana wa Mungu unirehemu mimi mwenye dhambi.