Nitajuaje kama nimeokolewa?

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Uhakika wa wokovu hauwezi kutegemea kazi yeyote ya mwanadamu, hisia na, matendo yake kwa sababu siku zote siyo kamili na zinaweza anayebadilika kila wakati. Usalama unaweza tu kutegemea kazi ya Mungu na ahadi zake.

Kwanza, Biblia inasema Mungu aliupenda ulimwengu na alifanya upatanisho na pamoja nasi kwa kusulubishwa kwa Kristo. Kwa hiyo Yesu alikuja kwa ajili yako pia.

Pili, kama umebatizwa umeunganishwa na kazi ya wuokovu ya Kristo. Hivyo wewe ni sehemu ya wokovu ambao ni ya ulimwengu wote.

Tatu, Biblia inafundisha kwamba atakaye amini na kubatizwa ataokoka.

Sehemu si katika nguvu za imani ila ni malengo yake: Kristo na ahadi za Mungu. Wakati sisi wenye imani havivu tunapomgeukia na kuomba msaada kutoka kwa Yesu hii inaitwa imani. Yesu anasamehe dhambi kwa sababu Biblia inaahidi “Yeyote atakayeliitia jina la Bwana ataokoka”. Imani pia zawadi kutoka kwa Mungu; Si uwezo na kazi ya mwanadamu mwenyewe. Hivyo basi kama umebatizwa na kurudi kwa Yesu na kuomba msamaha wa dhambi zako na kuomba wokovu, upo katika njia ya kwenda mbinguni.
Kwa kushiriki chakula cha Bwana na ahadi za Mungu ambazo umeunganishwa nayo kukupa nguvu na kuimarisha imani yako.

“Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu,nami hukaa ndani yake”.
(Yoh 6:54-56, SUV)