Je Mungu yupo?
Watu wengi hufikiri kwamba kwa njia fulani kuna Mungu, yaani nguvu na uwezo wa juu. Kuna anayeweka hufahamu juu ya mema na mabaya katika watu. Kuna anayeongoza hatima ya historia kwa mkono wake. Hata mtu asiyeamini Mungu ana sheria fulani “Mungu” ambaye anategemea na ambaye anayemwona kuwa mwenye mamalaka fulani.
Hisia tu na maoni au hakikisho juu ya uwepo wa Mungu haitwambii chochote kuwa Mungu ni nani , anaonekanaje, na jinsi tunaweza kumfahamu. Ujumbe kamili kuhusu Mungu unatoka kwake tu, neno lake katika Biblia. Mungu ni mkuu na amefichika na hatuwezi kufahamu kwa mawazo ya kibinadamu ambayo yana upungufu kwa sababu ya dhambi. Hii ndio sababu tunahitaji kuamini tangazo lake. Mungu aliuumba dunia na anaiongoza na kuitawala. Na zaidi sana–Mungu alifanyika mwanadamu katika Kristo Yesu hapa duniani na akatuondoa kutoka dhambi zetu. Hakuna mwingine na wala hakuna Mungu mwingine.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
(Ufunuo 1:8)