Roho Mtakatifu

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Biblia inatwambia kwamba kuna Mungu mmoja mwenye nafsi tatu; Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Na kila moja ya nafsi ina huduma yake. Mungu Baba aliumba ulimwengu na anaendelea kuutunza. Na Mungu Mwana alizaliwa katika mwili wa binadamu na kuaokoa ulimwengu kutoka katika dhambi. Roho Mtakatifu anaamsha na kujenga imani ndani ya mwanadamu. Kwa hiyo lazima tuulize “Roho Mtakatifu ni nani?" Kwa sababu Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu na wala sio nguvu inayojitegemea.

Roho Mtakatifu anafanya kazi kati ya mtu akiamsha na kuimarisha imani katika Yesu. Anafanya kazi kupitia vyombo vya Neema: neno la Mungu, Ubatizo na Meza ya Chakula cha Bwana (sacramenti) na ungamo la dhambi; hivi ni vyombo vya Neema.

Yesu alimwita Roho Mtakatifu “Roho wa Ukweli” na Mlinzi, kama Roho wa ukweli, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa Biblia kuandika katika mapenzi ya Mungu, na yeye anatupa kuelewa pale tunaposoma Biblia . Kama Mlinzi anatuhakikishia katika roho zetu kwamba Mungu ni wa rehema kwetu kupitia Yesu Kristo ijapokuwa tumeanguka na kustahili adhabu.

Ndani ya waamini Roho Mtakatifu anatoa uzima ambao unatokana na mapenzi ya Mungu na pia anatoa zawadi za Roho kulijenga Kanisa.

“Lakini ajapo huyo msaidizi nitakayewapelekea, kutoka kwa Baba, yaani Roho wa kweli, atokaye kwa baba yeye atanishuhudia"
(John 15:26, SUV)

Ombi: Mungu, niongoze kwako wewe.
Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Roho Mtakatifu anaweza kuishi ndani ya mwanadamu, hakika, kila muumini katika Yesu Kristo ana Roho Mtakatifu. Pasipo Roho Mtakatifu hakuna anayeweza kuamini. Mojawapo ya mambo yasiyoeleweka ya ukristo ni kwamba Mungu mwenye nguvu anatamani kuishi ndani ya moyo wa mwanadamu mdogo na mwenye dhambi.

Roho Mtakatifu anakuja kwenye moyo wa mwanadamu kupitia Neno la Mungu na kupitia sakramenti ya ubatizo na sacramenti ya Meza ya Bwana. Kwa Kutumia hivi vyombo vya Neema anaamsha imani ya kweli (uokoayo) ndani ya Yesu Kristo katika Moyo wa mwanadamu na kumfanya mtoto wa Mungu. Mtoto wa Mungu hata hivyo anaweza kukosa utii na kumhuzunisha Roho Mtakatifu na kuanguka katika kutoamini. Hii ndio maana Biblia inaonya kuhusu watu wenye mioyo migumu, na waasi na wanaojiinua, wapate kurudi tu kwa Mwokozi.

“Lakini Roho wa Mungu anakaa ndani yenu ninyi hamwufuati mwili, bali mwaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake”
(Warumi 8:9,SUV)

Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Wakati wasomi wanapinga kwamba Yesu alifanyakazi kwa kupitia nguvu za shetani, Yesu aliwaonya kuhusu kumkufuru Roho Mtakatifu. Kumkufuru Roho mtakatifu ni dhamira ya kinyume ya kazi za Roho Mtakatifu. Kuna mifano mahali pengine katika Biblia pia, katika barua ya kitabu cha Waebrania anazungumzia dhambi ya dhamiri ambaye ina kupelekea katika utengano na Mungu. Kwa njia hii haizungumzia dhambi nyingine ila ni dhambi inayokufanya ukatae imani.

Maneno ya Yesu katika waraka kwa Waebrania usieleweka kama kushutumu mtu yeyote lakini kama onyo kwa wale wote ambao hawajafanya dhambi hii. Ni muhimu kukumbuka kwamba mlango wa Mungu upo wazi kwa kipindi hiki ambacho injili ya Yesu Kristo inahubiriwa. Na shida kwa mtu ambaye alifanya dhambi ya kukufuru Roho Mtakatifu kwamba Mungu atasamehe au la! Lakini haya ni kutokuwa na mapenzi kumrudia Mungu – Moyo umefanya mgumu. Kwa hiyo yeyote anayeogopa kutenda dhambi ya kurudia anaweza kuwa na hakika kwamba hajafanya hiyo dhambi kwa sababu toba ni alama ya moyo ambao bado unaskiliza wito wa Mungu.

“Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa na katika ule ujao.”
(Mathayo 12:32,SUV)