Binadamu

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Machoni pa watu, uwezo wetu unaonakana katika uwezo tulio nao, hali zetu, pesa, mwonekano na kadhalika. Unaweza kujisikia kuwa wewe si mwema sana– hasa wakati maisha yako hayatimizi matarajio yanayotoka nje.

Dhamani yako ya msingi haitegemei hata hivyo mambo yaliyotajwa hapo juu. Hakuna mtu awaye yote anayeweza kutoa dhamani yako. Ni Mungu pekee aliyekuumba anayeweza. Hakukumba bure tu au kwa bahati mbaya ila kwa kusidi na upendo. Biblia inasema kuwa Mungu alimuumba mwadamu kwa mfano wake, mwenye dhamani kubwa kuliko vyiumbe vyote duniani.

Ulichorwa na kuumbwa na Mungu kuwa mototo wake mpendwa. Wewe ni mtu wa ina yake na hakuna mtu yeyote atakayechukua nafasi yako hapa duniani. Wewe una maana kubwa kwake – sana hadi akamtoa mwana wake afe msalabani ili kwamba uondolewe kutoka dhambi zako. Huitaji kulipia dhamani yako. Wewe unadhamani isiyo na kipimo kwa sababu umeumbwa, kupendwa na kuokolewa na Mungu.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.Matendo yako ni ya ajabu,Na nafsi yangu yajua sana
(Zaburi 139:14)

Ee Mungu, nibariki ili niweze kujiona jinsi unavyo niona.
Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mungu anakupenda – wewe hasa. Unaweza kujiuliza jinsi utakavyokuwa na uhakika juu ya hilo. Jibu ni raisi: Mungu mwenyewe anatuambia katika Bilia. Hasemi kwamba anawapenda watu wazuri na wema ila anapenda kila mmoja na wewe ni miongoni mwao.

Lakini unawezaje kuona upendo wa Mungu? Haonyeshi upendo kwa maneno tu ila pia kwa matendo. Tunapotazama aliyotutendea Mungu, tunaona jinsi upendo wake ulivyo mkuu. Mwanzoni kabisa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ulikuwa mkamilifu. Hawakuwa na mashaka juu ya upendo wa Mungu. Ila anguko na mwadamu liliharibu kila kitu na kuharibu uhusiano wetu na Mungu. Hata hivyo haikubadilisha upendo wa Mungu.

Upendo wa Baba yetu wa mbinguni ni mkuu kwamba alirekebisha hali hiyo. Upendo wake ulionekana miaka 2000 iliyopita wakati mwanae alikufa msalabani. Yesu alikufa ili usitenganishwe na Mungu kwa sababu ya dhambi zako. Yesu alikufa ili upate kufika mbinguni kuishi milele ukizungukwa na upendo wa Mungu.

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
(Yohana 3:16)

Mungu naomba nisikie upendo wako na kuuamini.
Mwandishi: 
Ville Auvinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Mungu ameahidi kusikia kila ombi lililo ombwa katika jina la Yesu. Kuomba katika jina la Yesu inamaanisha kwamba tunamwamini Yesu na hivyo tunaonganishwa na Mungu.

Mungu anasikia maombi yote, lakini haina maana kwamba atajibu kwa wakati wote kama unavyoomba au kutarajia. Mungu si mashine ya kujibu maombi yote ambayo yapo kwake, lakini ni baba anayejua mahitaji ya watoto wake.

Anatupa kile ambacho ni jema kwa mwanga wa maisha ya milele. Kwa hiyo wakati mwingine anayajibu maombi yetu kwa kukataa matakwa yetu. Anatufanya sisi kusubiri na wakati mwingine anatupa majibu thabiti.

Kwa hilo tunaweza kuwa na uhakika kwamba wakati tunapoomba msamaha wa dhambi zetu kwa wokovu mara moja anaharakisha majibu. Tunaweza kusoma majibu yake kwa Biblia alipotoa ahadi ya kusamehe dhambi kwa wale wanaoungama dhambi zao.

“Au kuna mtu yupi kwenu ambaye mwanawe akimwomba atampa jiwe?Au akiomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu ,manajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?"
(Mathayo 7:9-11 SUV)

Mungu wakati mwingine nashangaa kama unanisikia au la! Ahsante kwa kunisikia!