Je Mungu ni mwenye enzi?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Tunapoona ubaya na mateso yapo kwetu-pengine hata katika maisha yetu-inawezekana tukauliza wazo juu ya Mungu na mwenye enzi na Mungu mwenye upendo. Hata hapo tunaweza kugeukia neno la Mungu ambalo linaweza kutegemewa kuliko mawazo yetu ambayo yana upungufu.

Kulingana na Biblia Mungu ni Bwana wa mabwana na mfalame wa wafalme ambaye anatawala dunia nzima. Anaona na anajua kila kitu na hakuna chochote kinaweza kutendeka bila yeye kuruhusu. Kutokana na anguko la mwandamu, Shetani amepewa uwezo duniani. Hata hivyo nguvu zake haziwezi, wala kufika popote bila Mungu kuruhusu. Shetani tayari amepoteza maana an nafasi dhidi ya nguvu ya Mungu. Yesu alishinda nguvu za dhambi kupitia kwa kifo chake msalabani na kufufuka kwake.

Mara kwa mara ni vigumu kwetu kuelewa nia za Mungu, hata hivyo tunaweza kumwamini kuwa yeye nidye anaye ongoza yote. Mungu mwenye enzi anaona kikamilifu, Anajua yaliyo mema kwa ajili yetu. Mungu aliukmba ulimwemungu kwa nene la kinywa chake, na anaweza kuitunza. Na dunia yote inaweza kuona ukuu wa Mungu.

”Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.”
(Isaya 40:28)

Bwana, una nguvu zote. Naomba nipate kinga na matumaini katika nguvu zako.