Je chanzo ya maisha yametokana kwa bahati mbaya?

Mwandishi: 
Liisa Rossi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Fikiria juu ya compyuta au simu ambayo unatumia kusoma ujumbe huu. Je unaweza kumwamini mtu akikwambia kwamba chombo hicho kiko kama kilivyo kwa bahati wakati sehemu muhimu za hiyo simu zilikutana tu kwa bahati mbaya? Hata hivyo unajua mara moja kwamba mtu amepanga na kukitengeneza chombo hicho kwa sababu maalum? Dunia kunamoishi ndani yake je? Ni mtindo wa ajabu na wa kina sana kuliko chombo chochote kilichjotengenezwa. Mwili wa mwanadamu ni kitu cha ajabu ambacho unaweza kusitajabia. Kitu cha namna hii kisinge weza kuepo kwa bahati mbaya.

Kwa upande mwingine, dunia inaweza kuwa na machafuko, kugongana na hali ya mabariko. Hata hivyo, kuna Muumbaji wa ajabu nyuma ya kila jambo– na Baba mpendwa ambaye anajitambulisha kupitia Kristo. Dunia yote na kila mmoja wetu huishi kwa uwezo wa Munug. Aliumba dunia na kupangilia kila kitu kuwa viende sawa sawa. Hakuna kitu ambacho kiko kwa bahati tu, ila kwa kusudi kamili. Hakuna maisha ya mtu yeyote ambayo ni kwa bahati. Unaishi kwa sababau Mungu alikupanga uwepo. Misha yako yametokana na kusudi na mpangilio kamili na upendo mkuu.

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
(Mwanzo 1:1, 26-27, 31).

Mungu, fungua macho yangu ili nione vipaji vyako. Fungua midomo yangu ili nikushukuru na moyo wangu ukusifu.