Je naweza kumpata Mungu?
Kwa usahihi kabisa mtu hawezi kumtafuta Mungu,lakini Mungu ndiye anayemtafuta na kumpata mwanadamu. Mungu anaishi mahali pa juu sana mahali ambapo mwanadamu hawezi kufika, lakini yeye amekuja na kufanya kuwa karibu na sisi na kututafuta. Mungu amejifunua peke yake katika sakramenti, neno lake (Biblia) katika ubatizo na ushirika mtakatifu pia katika maungamo ya dhambi na masamaha ya dhambi. Katika hayo inatupasa kumtafuta huko.
Kama umebatizwa inakupasa kujikumbusha mwenyewe maana yake. Katika ukiri wa imani ya mitume na kateksimo ni mahali pazuri pa kuanzia kujifunza hata kama hujabatizwa ni vizuri kuanzia hapo. Na pia nakutia moyo kusoma Biblia, anza kusoma agano jipya na hasa INJILI.
Tafuta kanisa unaweza kuhiriki katika ibada ya jumapili. Kipindi cha ibada unaweza pamoja na ushirika kukiri na kuungama na kupokea tangazo la msamaha wa dhambi na kusikia mafundisho kutoka katika biblia. Kwa ushirika meza ya Bwana tunakuwa karibu na Mungu. Mungu anakutana nasi katika mkate na katika mvinyo- mkate ukiwa ni mwili wa Kristo na mvinyo ukiwa ni damu ya Kristo.
“Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika nitawatia nguvu wagonjwa nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu nitawalisha hukumu."
(Ezekieli 34:16, SUV)