Kuna Jehanamu?

Mwandishi: 
Pasi Palmu
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ndio ipo. Agano la kale linasema kwa kina kuhusu mahali baada ya kufa, lakini kati ya kipindi cha Agano jipya inatoa mwanga hata katika ukweli wa giza hili. Yesu alisema jehanamu haikuumbwa kwa ajili ya mwanadamu ila ni kwa ajili ya shetani na malaika zake. Unaelezewa kama Jehanamu ya moto wa milele, ziwa la moto Giza, utengano, kilio na kusaga meno. Wakati hatuwezi kuelezea ni vipi tunafikiri kuhusu mtazamo wa kuzimu, tunaweza kutazama katika tafsiri hii: Kuzimu na utengano wa milele na Mungu na uzuri wote wa Mungu. Mkristo hatakiwi kuwa na mvuto wa kuzimu, zaidi sana uepuke kuwa huko. Tunatakiwa kukumbuka kuwa Yesu hakuja katika ulimwengu huu kutuogopesha kuhusu kuzimu bali kutukomboa kutoka ajili ya kwenda Mbinguni. Wewe pia!

“Kisha atawaambia na wale waliopo mkono wake wa kushoto, ondokeni kwangu, mliolaaniwa mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilishi na malaika zake.”
(Mathayo 25:41, SUV)