Nani anastahili kushiriki meza ya Bwana?
Ushirika mtakatifu ni kwa wakristo waliokwisha kubatizwa. Katika Kanisa la Kilutheri wale wote waliokwisha kwenda katika kipaimara na wameshabarikiwa wanaweza kupokea ushirika mtakatifu. Hivi ndivto inaweza kuhakikishwa kuwa washirika wameelewa maana ya ushirika mtakatifu na kujua tofauti ya ushirika mtakatifu na kula na kinywaji cha kawaida. Pia watoto waliofundishwa wanaweza kupokea meza ya Bwana pamoja na wazazi au wazee wao. Na kila mmoja anaweza kuja madhabahuni kubarikiwa.
Wakati mwingine unaweza kujihisi vigumu kwenda kwa meza ya Bwana. Mwingine anweza kujisikia kwamba wema wake hautoshi kupekea sakramenti, kwamba lazima awe mwenye imani imara. Hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe. Meza ya Bwana si kwa ajili ya uzuri wetu tulionao au kwa wale waliofanikiwa kaika maisha. Kinyume chale meza ya Bwana ni kwa wale wote wanohitaji msamaha wa dhambi. Katika ushirika mtakatifu rafiki na mkombozi ana rehema kwa wale wote walioshindwa. Ushirika mtakatifu ni kwa wale wote wanaohitaji msamaha wa dhambi. Meza ya Bwana si kwa wale wote wanofikiri kuwa hawamwitaji Yesu Kristo.
Biblia inatuonya sisi juu ya kwamba mtu anaweza kula na kunywa mwili na damu ya Yesu kwa hukumu yake mwenyewe. Baadhi ya watu ambao onyo hili lilipewa, kwa asili ni wale ambao kupokea meza ya Bwana na hawakufikiri kwamba ni ushirika mtakatifu. Walikula na kunywa hata kulewa . na mkate na mvinyo viliweza kuliwa bila utaratibu. Paulo aliandika kwamba ambaye anapokea ushirika mtakatifu na hajui ni mwili wa Kristo, atakuwa anakula na kunywa hukumu yake mwenyewe. Onyo hili mara nyingi limeeleweka vibaya, na kukataa ushirika mtakatifu kwa wale wote ambao si wema, na imani zao ni dhaifu. Lakini hii si maana yake.
“Maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.”
(1 Korintho 11:26 SUV)