Meza ya Bwana ni nini?
Wakristo wanashiriki meza ya Bwana (Ekarisiti) kama Yesu alivyoamuru. Kila wakati wote wanaposhirikishwa, maneno ya Yesu yanayofanya Ushirika mtakatifu yanasomwa. Meneno yake yamechukuliwa kutoka katika maandiko matakatifu ya Biblia ambayo yanasemwa nini kilitokea Yerusalemu usiku kabla ya kifo cha Bwana Yesu. Yesu na wanafunzi wake walisherehekea sakramenti ya meza ya Bwana, na Yesu aliwaambia waendelee kufanya hivyo baadaye.
Katika maneno ya Meza ya Bwana yanasema kwamba mkate ambao tunaumega ni mwili wa Bwana Yesu na mvinyo ni agano jipya katika damu yake. Katika ya Mathayo, Yesu alisema pia ni damu yake. Vivyo hivi mwili na damu vipo katika meza ya Bwana inashirikishwa. Ina maana kwamba Yesu yupo ndani ya mkate na mvinyo kwa njia maalum. Tunakutana naye naye anakutana na sisi. Unapofikiri utakuwa karibu na Yesu, nenda shiriki katika meza ya Bwana. Huu ni muujiza mkubwa wa meza ya Bwana. Yesu yuko pale na anafanya kazi ndani yetu.
Katika ushirika mtakatifu mara nyingi unaweza usihisi kana kwamba untakutana na Yesu. Lakini mawazo yetu hayawezi kumzuia Yesu kuja karibu yetu. Yeye yupo pale alipoahidi kuwa na haijalishi tunafikiri. Aliahidi kuwa katika meza ya Bwana-Mkate ni mwili wake, ana mvinyo ni damu yake.
"Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa Mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni mle; huu ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki, kwa maana hii ndio damu yangu ya agano, imwagikayokwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."
(Mathayo 26:26-28, SUV)