Je nisipo samehe?
Kusamehe kunaweza kuwa vigumu na pengine kutowezekana. Si hoja, katika Biblia tunatiwa moyo kuomba msamaha na kusamehe. Kwa kweli, inetamkwa kwa nguvu kwamba hatutasamehewa kama hatutasameheana.Tufanye nini basi, wakati hatuwezi kusamahe na uchungu unasumbua moyo?
Kwa kabisa, ni muhimu kwamba tuweze kukiri dhambi hii mbele za Mungu. Tulete ukweli huu mbele zake kwamba tunmeshindwa kusamehe. Kwa ajili ya Yesu tunaweza kuamini kuwa hata dhambi hii imesamahewa. Wakati huo huo tuombe kwamba Mungu kwa neema yake anaweza kufanya kazi yake ndani yatu na atuzaidie tuweze kusamahe. Ni kwa msaada wa neema yake tu vidonda katika mioyo yetu vinaweza kupona kabisa. Mazungmzo na mwanasaikogia au mchungaji au mtu aliyetukosea inaweza kuwa msaada mwema.
Kusamehe ni uamzi tunauchukua. Kama hali, msamaha unaeza kuwa hata hivyo hatua ndefu. Inaweza kuchukua hata miaka ili kuweza kuwa huru kutokana na uchungu. Hata hapo ni muhimu kuachilia hali ya kulipisa kisasi.
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
(Waefeso 4:32)