Utatu ni kati ya misingi
Wakristo wanaamini katika Mungu mmoja, ambaye ni Baba Mwana na Roho mtakatifu. Neno “utatu” kwa asili limekuwa likitumika wakati tunaposema kuhusu Mungu, ijapokuwa Biblia haijatumia msemo huo. Kifungu hiki cha imani ni cha muhimu kwa kanisa kwamba, yeyote anayepinga kwa asili aeleweka kama si mkristo. Lakini hii ina maana gani katika yote?
Kusudi la huui utangulizi mfupi si kuchukua umuhimu wa hili somo kwa kina kama unavyohitajika, maelezo mengi juu ya imani ya Kikristo, zilizoandikwa na wanahistoria wa kanisa, mfano kazi ya umakini ya baba wa kanisa Augustino aliyoifanya. Hata hivyo uwasilishaji ulishughulika tu na msingi ambao pia ulikuja jinsi tulivyo nao.
Mahali pa kuanzia
Tokea mwanzo, wakristo wamekuwa wakikiri imani ya agano la kale, kuna Mungu mmoja. Ilikuwa na ukiri wa Israeli mfano Paulo mtume alikuwa anahusika katika hilo.
”sikiliza Ee Israel, Bwana wetu ndiye mmoja.”
(Kumbukumbu la torati 6:5 SUV)“Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingine na mabwana wengi, lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu aliye Baba ambaye vitu vyote vimetoka kwake nasi tunaishi kwake, yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwepo na sisi kwa yeye huyo.”
(1 Kor 8:5-6 SUV)
Wakati agano jipya lote linaelezea kanuni za msingi pia inazungumzia kuhusu Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.
“Yesu akaja kwao akasema nao akawaambia, nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari.” (Mathayo 28:18-20 SUV)
“Neema ya Bwana Yesu Kristo na pendo la Mungu na ushirika wa Roho mtakatifu ukae nanyi nyote.”
(2 Kor 13:14 SUV)
Hivyo kuna Mungu mmoja lakini tunazungumzia kuhusu Baba, Mwana na Roho mtakatifu, mitazamo yote lazima iwe katika akili.
Baba ni Mungu, na Kristo ni Mungu na Roho mtakatifu ni Mungu
Nina bahatisha hakuna hata mmoja ambaye anasoma Biblia anauliza uungu wa Mungu. Agano jipya pia kwa usahihi linafundisha kwamba Yesu Kristo Mwana wa Mungu ni Mungu.
“Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote, Mungu mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndyie aliyemfunua.”
(Yohana 1:18 SUV)“Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba, tumjue yeye aliyewa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.”
(1 Yohana 5:20 SUV)“Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.”
(Wakolosai 2:9 SUV)
Tayari ndani ya agano la kale kumetajwa kuhusu Roho wa Mungu ambayo aliwapa watu wake:
“Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, name nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nam nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu,nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda.”
(Ezekieli 36:26-27 SUV)Kwa mfano kitabu cha waefeso kwa usahihi kinaeleza kwamba si nguvu inayovuta vitu chini, vinginevyo vingeumiza lakini ni nafsi, maelezo kutoka kwa kitabu cha waefeso, “wala msimhuzunishe Yule Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.”
(Waefeso 4:30 SUV)
Kitabu cha matendo ya mitume kinatueleza juu ya Anania na Safira walivyomdanganya Roho mtakatifu- kwa namna nyingine Mungu- na kupata hukumu waliyostahili.
“Petro akasema, Anania,kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uwongo roho Mtakatifu na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?”
(Matendo ya mitume 5:3 SUV).
Hivyo Baba ni Mungu na Kristo ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu. Na wote ni Mungu mmoja anayeishi, kuna Mungu mmoja lakini mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu anayejidhihirisha kwa kila mmoja kwa watu wake.
Binti mmoja aliyepata kuokolewa alituuliza kwa njia ya kuchanganyikiwa kama angetakiwa kuomba kwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, bibi yake alimpa jibu rahisi lakini la kutuliza moyo wake. Omba kwa mmoja kati yao. Watakubaliana kwa pamoja nani atakuja na kukusaidia. Kuthibitisha huu mkanganyiko wa ushauri, acha atufungue Biblia.
Kutokana na Mwana wa Mungu Yesu, hatuwezi kumjua mwana pasipo Baba.
”wakati ule Yesu akajibu, akasema nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili ukawafunulia watoto wachanga.”
(Mathayo 11:25 SUV)“Yesu akajibu akmwambia heri wewe Simoni Bar-Yona, kwakuwa mwili na damu havikukufunulia hili bali baba yangu aliye mbinguni.”
(Mathayo 16:17 SUV)
Kwa upande mwingine hatutaweza kumjua Baba pasipo Yesu.
“Akasema, nimekabidhiwa vyote na Baba yangu wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba wala hakukna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”
(Mathayo 11:27 SUV)“Yesu akamwambia mimi ndimi njia na kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.”
(Yohana 14:6 SUV)
Hakuna hata mmoja anaweza kuguswa na Mungu pasipo Roho Mtakatifu
“Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu bali mlipokea Roho ya kufanywa wana amabayo kwa hiyo twalia Aba, yaani Baba.”
(Rumi 8:15 SUV)“Kwa hiyo nawaarifu yakwamba hakuna mtu anenaye katika roho wa Mungu kusema Yesu alilaaniwa wala hawezi m tu kusema Yesu ni bwana isipokuwa katika Roho Mtakatifu.”
(1 Kor. 12:3 SUV)
Hivyo Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wanatukuzwa kila mmoja kwetu.
Ni vipi tunaweza kuanza kuelewa hii
Katika kitabu chake kizuri “Habari njema kwa wakristo wa Anxious” Philipo Carey alinakili maelezo saba ya msingi ya Augustino.
- Baba ni Mungu
- Mwana ni Mungu
- Roho Mtakatifu ni Mungu
- Mwana si Baba
- Mwana si Roho Mtakatifu
- Roho Mtakatifu si Baba
- Kuna Mungu mmoja tu
Maelezo haya yako sambamba na biblia kwa msaada wao tumeanza kuelewa swali. Kuna Mungu mmoja, mwenye nafsi tatu. Hatuwezi kamwe kuingia ndani zaidi katika asili ya Mungu kwani yeye ni siri kubwa, kwa taadhari tuatmwelewe yeye katika sehemu ndogo ambayo alijifunua nayo kwetu. Baada ya kuelewa baadhi ya maelezo ya msingi kuna mengi ya kushangaa, mengi zaidi yanaweza kuwa yamesemwa na pia yanaweza kuwa yamefundishwa na kuwakilishwa kwa ujazo zaidi. Lakini natumaini umepata mahali pazuri pa kuanzia kwa hili moja.