Mtu anaweza kuokolewa pasipo ubatizo?
Biblia inasema kwamba ili uokolewe unahitaji ubatizo na imani. Lazima tuwe macho ni nini Mungu alisema kuhusu hilo. Vinginevyo tutakuwa hatarini kuachwa nje ya kazi yake ya ukombozi. Kwa hiyo lazima tuwabatize watoto wetu na kupokea ubatizo sisi wenyewe kama bado hatujabatizwa.
Biblia inasema kwamba baadhi ya watu waliookolewa pasipo kubatizwa. Katika ijumaa kuu, Yesu alisema kwa yule mwaalifu aliyekuwa karibu yake kwamba atakuwa pamoja naye paradiso. Huyu mtu alikuwa hajabaptizwa. Mungu anaweza fanya kazi hata nje ya vyombo vya neema ambavyo ametuambia kuvitumia. Anaweza kuokoa hata bila ubatizo. Lakini mtazamo huu wa kiuungu hauturuhusu sisi, kudharau ubatizo ambao ametuamuru sisi tuupokee. Kama wakristo tumefungwa katika mafundisho ya Agano jipya: Katika ubatizo tunafanyika kuwa wakristo na watoto wa Mungu. Wakati mtoto aambaye hajabatizwa akifa tunaweza kusema tu kwamba yeye yuko mikononi mwa Mungu wetu mwenye Rehema.
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa.”
(Marko 16:16 SUV)