Nitawezaje kuanza kusoma Biblia?

Mwandishi: 
Erkki Koskenniemi
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Njia nzuri ya kusoma Biblia ni kuanza kusoma mojawapo ya vitabu vya injili kutoka mwanzo hadi miwsho. Changuo linaweza kuwa ngumu kwa sababu injili zote zina tabia zao mbali mbali. Ukichagua uzuri wa Marko usiorembeka− mistari yake mikafu huifanya ifutie. Au ukichagua injili ya Yohana na kuingia katika urembo wenye joto ambao inaoaka rangi? Chaguo lolote ambalo utaamua, anzia injili, some zote na halafu halafu endelea na Agano jipya kwa mpangilio. Kitabu kimoja kwa wakati moja tangu mwanzo hadi miwsho, kila siku kulingana na uwezo wako.

Kwa mfano ukisoma Agano jipya mara mbili unaweza kuendelea na Agano la Kale. Vitabu wa kwanza vya Musa vinaweza kupatikana kwa uraisi lakini baada ya hivyo unaweza kushangaa juu ya amri ambazo zilipewa kwa watu ambao si Wayahudi. Ikifika upande wa manabii, jambo la maana ni kujifunza lini na katika mazingira gani kitabu kiliandikwa. Kwa hili utahitaji msaada zaidi. Ila si usumbufu wa bure- Agano la kale nimejaa hazina ambazo zinafaa kupatikana!

Kila neno la Mungu limehakikishwa;Yeye ni ngao yao wamwaminio. (Mithali 30:5)