Ni kweli Yesu alifufuka kutoka kwa wafu?

Mwandishi: 
Sirkka-Liisa Huhtinen
Mtafsiri: 
Richard Ondicho Otiso

Ni sehemu mbili zinatueleza tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?

Matukio mawili ya mazimulizi yamezungumziwa tangu mwanzo – ni ipi unayoiamini?
Injili ya Mathayo inatuambia jinsi walinzi katika kaburi la Yesu walipewa rushwa na kupewa maelezo ya kusema kwamba wanafunzi wake walikuja usiku na kuiba mwili wa Yesu. Uongo huu unaendelea hata leo na unaendelea kuboreshwa na kuwa kisasa. Maelezo ya leo ni kwamba kifo cha Yesu kilisababisha mkanganyiko wa kiakili kwa wanafunzi. Hivyo njia moja tu ya kuendelea kuishi ni kutengeneza imani, kuamini kwamba Yesu alifufuka katika wafu na kupitia imani anaishi katika roho.

Agano jipya hata hivyo linatuambia kwamba kuna watu wengi waliokutana na Yesu katika hali ya kimwili. Wanawake katika kaburi, wanafunzi waliokuwa wamefunga milango kwa hofu, watu wawili katika safari ya Emau n.k. Tomaso mwenye mashaka alipata nafasi ya kugusa majeraha ya Yesu. Watu hao wote walikuwa na vitu vinavyofanana: walikuwa na muda mgumu wa kuelewa na kukubali kwamba hakika Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.

Baada ya kufufuka kwake Yesu hakujionyesha kwa washtaki wake au ulimwengu mzima ni kaburi tupu tu ndilo lilidhihirisha hivyo. Mwili wake haukuwepo kaburini.

Hakuna kazi ya kuweza kuhakiki hiyo kazi au kutoa sababu ambayo inaweza kumshawishi mtu kuhusu ufufuko wa Yesu- imani huja unapokutana na Yesu. Yesu yuko mbinguni na baba yake, lakini neno lake-Biblia linazidi kuzungumza na watu ulimwenguni. Kanisa lake ni hakikisho kwamba Yesu yu hai.

”Yesu akamwambia kwa kuwa wewe umeniona, umesadiki; waheri wale waio ona wakasadiki.”
(Yohana 20:2a SUV)

Ombi: Yesu wasema kwamba unaishi. Unanisikia ninapoomba?