Nini kitatokea kama sikubatizwa?
Wewe unayependa mambo ya imani na hujabatizwa unaweza shangaa kama utatakiwa kubatizwa. Naam unahitaji. Wasiliana na mchungaji au mfanyakazi wa usharika wa kanisa la Kilutheri. Pamoja na mchungaji mnaweza kwenda moja kwa moja katika mafungu muhimu ya imani na baadaye unaweza kubatizwa,au ungelipenda kubatizwa lakini si rahisi labda uko chini ya umri wa mika 15 au wazazi wako hawapendi wewe ubatizwe. Unaweza kumwanini Yesu ijapokuwa hujabatizwa. Omba ubatizwe mara tu kama ulivyoamua.
Labda una mtoto mdogo ambaye hajabatizwa? Inafaa mtoto huyu abatizwe? Ndiyo. Wasiliana na mchungaji au mfanyakazi wa usharika na mpange ubatizo.
“Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpaate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapoke kipawa cha Roho mtakatifu kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu walio mbali na kwa wote watakaitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
(Matendo ya mitume 2:38-39 SUV).